
Mbali na jukumu nyeti la uzinduzi wa Bodi, Afisa Elimu Mkoa, katika uzinduzi huo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa:
1. Bodi ni takwa la kisheria.
2. Kila mjumbe wa Bodi atimize majukumu yake ipasavyo.
3. Ni jukumu la Bodi kumshauri mwenye shule ipasavyo.
4. Kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya serikali.
5. Bodi ni sikio na mdomo wa mwanafunzi, ndicho chombo cha kumsikiliza na kumsemea kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizowekwa